19 Machi 2011 - 20:30

Waasi wa Sudan Kusini wamesema kuwa wataendelea na mapambano yao dhidi ya serikali ya Juba licha ya kuuawa kiongozi wao George Athor.

Habari kutoka Juba zimemnukuu msemaji wa waasi hao, James P. Rubin, akisema kuwa wataendelea na mapambano yao dhidi ya serikali ya Sudan Kusini.Itakumbukuwa kuwa juzi Jumatatu, Riek Machar, Makamu wa Rais wa Sudan Kusini alitangaza habari za kuuawa George Athor pamoja na walinzi wake kadhaa katika mapigano yaliyotokea kwenye eneo la mpakani la Comte de Morobo.Philip Aguer, msemaji wa jeshi la Sudan Kusini amesema kuwa, mwili wa Athor ulipangiwa kupelekwa Juba leo Jumatano.George Athor alikuwa afisa wa ngazi za juu katika jeshi la SPLM la Sudan Kusini lakini alijitoa jeshini na kuongoza uasi dhidi ya serikali ya Juba baada ya kusema kuwa kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi wa 2010.